IQNA

Watoto watatu wenye ulemavu wa macho Misri wahifadhi Qur’ani + Video

13:37 - March 10, 2018
Habari ID: 3471424
TEHRAN (IQNA)- Watoto watu wa familia moja wamehifadhi Qur’ani kikamilifu nchini Misri pamoja na kuwa wamezaliwa wakiwa na ulemavu wa macho.

Ndugu hao watatu, wawili wa kiume na moja wa kike kutoka mkoa wa Beni Suef, wameweza kuhifadhi kikamilifu na hivyo kuthibitisha kuwa sahihi ule msema usemao kuwa ‘Ulemavu sio ukosefu wa uwezo.’

Moja kati ya watoto hao wenye ulemavu wa macho ambaye yuko katika shule ya msingi anasema: “Kila wakati ninapotoka shuleni na kurejea nyumbani, hujishughulisha na kuhifadhi Qur’ani na kusikiliza tilawa ya aya za Qur’ani.”

Anasema wazazi wake wamempa motisha sana na ni moja ya sababu za mafanikio yake katika kuhifadhi Qur’ani Tukufu.

Baba mzazi wa watoto  hao watatu wenye ulemavu wa machi anasema: “Qur’ani Tukufu inamjenga mwanadamu name  nimejaza mahaba ya Qur’ani katika nyoyo za watoto wangu tokea wakiwa wachanga.”

Wakati huyo huo shirika moja la misaada Misri limetangaza mpango wa kuwasaidia watoto hao wafanyiwe upasuaji ili kuboresha uwezo wa macho yao. Kwa maelezo zaidi sikiliza au tizama klipu ya video inayofuata hapa chini.

3697807

captcha