IQNA

Mashindano ya Qur'ani ya wenye ulemavu nchini Misri

11:48 - March 05, 2018
Habari ID: 3471417
TEHRAN (IQNA) – Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu Marekani inapanga kuandaa mashindano ya Qur'ani kwa watu walemavu na wale wenye mahitajio maalumu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, taarifa ya wizara hiyo imesema mashindano hayo yamepangwa kwa wale walio katika umri wa chini ya miaka 25.

Mashidano hayo yatakuwa na kategoria tatu zikiwemo kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, kuhifadhi juzuu 15 na kuhifadhi juzuu tatu za mwisho za Qur'ani. Washiriki pia watashindana katika kufahamu maana ya aya za Qur'ani.

Kati ya masharti kwa washiriki ni kuwa wasiwe waliwahi kushika nafasi za tatu za kwanza katika mashindano yaliyaondaliwa na wizara hiyo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.

3696097

captcha