IQNA

Kijana wa miaka 20 ashinda mashindano ya Qur'ani Nigeria

11:33 - March 05, 2018
Habari ID: 3471416
TEHRAN (IQNA) – Kijana mwenye umri wa miaka 20, Amiru Yunusa, wa Jimbo la Bauchi ametangazwa kuwa mshindi wa Mashindano ya 23 ya Kitaifa ya Qur'ani ya Nigeria yaliyofanyika katika jimbo la Katsina kaskazini mwa nchi hiyo.

Aidha, Amina Ahmad wa Jimbo la Borno ametangazwa mshindi katika kitengo cha wanawake katika mashindano hayo ya kitaifa.

Dkt. Sani Yunus Birnin-Tudu, mratibu wa kitaifa wa mashindano' alitangaza matokeo hayo siku ya Jumamosi na kusema washiriki walishindana katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu. Aidha aliongeza kuwa mashindano hayo yaliwajumuisha washiriki 360 kutoka majimbo 32 ya Nigeria na yaliendelea kwa muda wa wiki moja.

Dkt. Birnin-Tudu amesema washindi wamatunukiwa zawadi mbali mbali kama vile magari mapya, Qur'ani za kidijitali, laptopu na fedha taslimu.

Akizungumza katika hafla hiyo Profesa Abdullahi Zuru Mkuu wa Chuo Kikuu cha Usmanu Danfodio cha Sokoto, ambacho kiliandaa mashindano hayo, amepongeza Serikali ya Jimbo la Katsina kwa kuwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ambayo yalifana.

3465316

captcha